Musa Mwarabu aliishi miaka mingi ya karne ya 4 kama mkaapweke maarufu kati ya Misri na Syria,[1] kabla hajafanywa askofu wa kwanza wa Kiarabu kati ya Waarabu kutokana na sharti la malkia wao, Mavia, kwa ajili ya kusimamisha mapigano yake na Dola la Roma.[2]
Kama askofu Musa hakuwa na makao maalumu, bali alifuata tabia ya uhamaji wa watu wake, akiwaongoa wengi na kudumisha amani kati yao, tena kati yao na dola hilo.[1]
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Februari[3][4].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search